Ndugu, Mzazi/Mlezi Uongozi na Menejimenti ya Msolwa “St. Gaspare Bertoni” Sekondari , unakutaarifu kuwa kikao kilichokuwa kimepangwa kufanyika tarehe 14/08/2021 kimeahirishwa kutokana na mlipuko wa UVIKO-19. Utawala wa shule umezingatia agizo la Serikali la kuzuia mikusanyiko yoyote kama sehemu ya tahadhari ya ugonjwa tajwa. Hivyo, kikao hicho kimeahirishwa mpaka hali itakapo kuwa shwari. Asanteni, tunawatakia kazi njema